Jumatatu, 20 Aprili 2015

TARATIBU ZA KUFUATA TBS KWA WANAOTAKA KUPIMA SAMPULI ZA BIDHAA

  • ANDIKA BARUA KWA MKURUGENZI MKUU UKIOMBA KUPIMIWA SAMPULI YAKO NA VIPIMO UNAVYOTAKA VIPIMWE
ANUANI:
MKURUGENZI MKUU,
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS),
S L P 9524, DAR ES SALAAM
TANZANIA
Baruapepe: info@tbs.go.tz
  • WASILISHA BARUA YAKO TBS KWA MKONO, AU TUMA KWA NJIA YA POSTA AU KWA NJIA YA MTANDAO
  • MTEJA ATAJULISHWA GHARAMA ILI AWEZE KULIPIA, KIASI CHA SAMPULI INAYOTAKIWA KUWEZESHA UPIMAJI NA TAREHE AMBAYO MAJIBU YATAKUWA TAYARI KUCHUKULIWA
  • MTEJA ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI KWA ASILIMIA MIA MOJA (10%) NA ATAPEWA STAKABADHI MBILI ZA MALIPO HALISI NA NAKALA YA STAKABADHI
  • MTEJA ATAWASILISHA NAKALA YA STAKABADHI YA MALIPO KATIKA OFISI YA KUPOKELEA SAMPULI
  • SAMPULI TAPOKELEWA KATIKA CHUMBA CHA KUPOKELEA SAMPULI
  • SAMPULI TAPELEKWA MAABARA NA WATUMISHI WA TBS
  • UPIMAJI UTAANZA NA KUKAMILIKA KATIKA MUDA ALIOJULISHWA MTEJA
  • MTEJA ATACHUKUA RIPOTI YA VIPIMO BAADA YA KUONYESHA NAKALA HALISI YA STAKABADHI KATIKA OFISI HUSIKA
(Taarifa ya TBS)

Jumatano, 21 Januari 2015

Driver missing in a computer(solution)


Somalia Lugha za kigeni marufuku,ofisini

Raisi Hassan Shaykh Mahmud alikuwa akizungumza hayo katika sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 42 tangu kuanza kutumika kwa lugha ya Kisomali nchini humo ,maadhimisho yaliyofanywa mjini Mogadishu kwa lengo la kutaka kuiimarisha lugha hiyo.Hata hivyo maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mamabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini humo. Matumizi ya lugha ya kisomali katika ofisi za serikali yametakiwa kuanza January mosi mwaka huu na kuendelea.Shughuli zote za kiserikali nchini humo zimetakiwa kuendeshwa katika lugha ya kisomali na si lugha ingine yoyote.Ruhusa ya matumizi ya lugha za kigeni imetolewa tu wakati wageni kutoka nje ya somalia watakapo kuwa wakihudumiwa . Hata hivyo waziri wa habari wa taifa hilo,ametilia mkazo kauli hiyo na kudai kwamba January 21 ni siku muhimu sana kwa taifa hilo,na siku hiyo ni kumbu kumbu kwa gazeti la kisomali la kwanza kuchapishwa.naye spika wa bunge la Somalia,Muhammad Shaykh Usman Jawari,ambaye pia alitoa kauli yake kwenye maadhimisho hayo,na kusema kwamba ni jambo muhimu kwa jamii ya wasomali kuelewa umuhimu wa lugha yao na kuitaka jamii kuiimarisha lugha hiyo. Rais Mahmud aliongeza kusema kwamba tarehe 21 January ni siku muhimu kwa wasomali na serikali yao.

SPLM kumaliza mgogoro Sudan Kusini

Viongozi walioshuhudia utiwaji saini makubaliano ya kusitisha mapigano. Makundi yanayopingana nchini Sudan Kusini yamekusanyika nchini Tanzania kusaka jitihada mpya za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusababisha maelfu ya watu kuuawa. Serikali ya Tanzania ambayo inasimamia mazungumzo ya Arusha kupitia chama tawala cha CCM nchini humo, imesema Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na aliyekuwa naibu wake na sasa kuwa kiongozi wa waasi nchini humo Riek Machar walikutana Jumatano na kutiliana saini mkataba mpya wa amani. Pande mbili hizo zilitiliana saini mkataba unaolenga kukiunganisha chama tawala cha the Sudan People's Liberation Movement (SPLM), ili kumaliza uhasama uliojitokeza miongoni mwa viongozi wa chama hicho kilichopigania uhuru wa Sudan Kusini miaka mitatu iliyopita. Vita vilizuka nchini Sudan Kusini, taifa changa kuliko yote duniani, mwezi Desemba 2013 wakati Kiir alipomshutumu naibu aliyemfukuza Machar kwa jaribio la kumpindua. Mara ya mwisho Kiir na Machar walikutana mwezi Novemba, 2014 mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako walikubaliana kusitisha haraka vita, mkataba uliovunjwa katika muda wa saa chahche tangu wakubaliane. Mapigano katika mji mkuu wa Juba yamesababisha mauaji ya kulipiza kisasi nchini humo na kuisukuma nchi kuingia katika kipindi cha njaa. Shughuli za kutiliana saini mkataba wa amani kati ya Rais Kiir na Bwana Machar zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kikanda kushuhudia mkataba wa umoja kw makundi tofauti ya chama tawala cha SPLM. Mazungumzo ya Tanzania yanafanyika sambamba na juhudi za kuleta amani zilizokuwa zikisimamiwa na nchi za IGAD mjini Addis Ababa, Ethiopia. Awamu nyingine ya mazungumzo ya IGAD yanatarajiwa kufanyika kando ya kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa mwishoni mwa Januari. Lakini vita vinaendelea. Wiki hii msemaji wa jeshi Philip Aguer amesema jeshi na waasi wamekuwa na mapigano makali katika jimbo la Central Lakes, na ameshutumu majeshi ya Machar kwa kulipua kisima cha mafuta katika jimbo la Unity. "Majeshi ya Machar yamekuwa yakisababisha uharibifu, uchomaji wa vijiji, uharibifu wa visima vya mafuta," amesema. Ni mara ya kwanza waasi mahasimu hao kukutana tangu waliposaini makubaliano ya kuacha mapigano mwezi Agosti huko Ethiopia, ambayo kama mikataba mitatu iliyopita ilivunjika mara moja. Viongozi hao wa siasa na kijeshi wamekuwa wakirudia rudia kuvunja ahadi wanazotoa chini ya msukumo wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Sudani ya Kusini uliofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Waziri Mkuu wa Marekani John Kerry. Safari hii viongozi hao wawili wa Sudani ya Kusini walisema chama tawala kilichogawanyika, Sudan People's Liberation Movement (SPLM), inapaswa kuungana upya. Chama cha SPLM kiliiletea nchi uhuru baada ya vita vya muda mrefu na Khartoum. "Chama kilichogawanyika cha SPLM kitaigawa nchi katika makundi ya kikabila na maeneo," makubaliano hayo yalieleza, kutoa wito kwa "mazungumzo ya halali na ya uaminifu ambayo yanaweka matakwa ya watu na taifa juu ya wote". Kiir alitoa ahadi ya "utatuzi kwa amani wa mgogoro" katika nchi iliyokuwa maskini wakati ina utajiri wa mafuta, ambayo ina miaka mitatu lakini iliyokumbwa na vita. "Hakuna sababu kwa watu wetu kupata shida tena baada ya uhuru," alisema. Machar pia alisema alitaka jambo hilo kumalizika. "Hatutaki fursa hii kutoweka kama fursa nyingine za awali," alisema. "Tutafanya kwa uwezo wetu wote kuona kuwa mchakato huu unamalizika" Kikundi cha tatu kilichojitenga katika SPLM -- viongozi wa ngazi ya juu walifungwa kwa miezi kadhaa baada ya vita kuibuka mwezi Desemba, lakini pia walisaini suala hilo la kuunganisha chama.